Na Evaline Komba - Maisaka Katani
Kamati ya Mipango Miji chini ya Mwenyekiti Mhe. Ramadhani Ammi imeridhia ombi la Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini [RUWASA] la kuuziwa viwanja kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba za watumishi wenye thamani ya shilingi 19,048,000/= wametoa ridhaa hiyo walipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa eneo la kitalu RR Maisaka Katani.
Kamati imeridhia ombi la viwanja hivyo wauziwe RUWASA kama walivyopendekeza kwa kuwa Ofisi zao zimejengwa maeneo hayo na Mji utaendelea kukuwa na kupendeza zaidi na wananchi imewasaidia kwa namna moja ama nyingine kwa kusogezewa huduma karibu zaidi.
Sambamba la hilo kamati imepata elimu juu ya kuondoa magugu maji na huku wakimtaka Afisa mazingira kuandaa nguvu kazi kwa ajili ya zoezi hilo la kuondoa magugu maji katika Ziwa Babati ili kuleta muonekano mzuri wa Ziwa na kuzidi kuwa kivutio.
Ziara hiyo imelenga kukagua eneo la Ziwa Babati ambalo limeathiriwa na magugu maji pamoja na viwanja ambavyo awali ilikuwa ni barabara ya mchepuko.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati