Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mh.Kibiki M. Kibiki amezindua rasmi bodi ya huduma za afya na kamati ya usimamizi ya Hospitali ya Mji wa Babati (Mrara) siku Jumatatu ya tarehe 30/10/2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Babati.
Kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mrara Dkt.Charles Mtabho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji alitoa maelezo kuwa bodi na kamati hizo zimeundwa kufuatia kuisha muda wake mnamo mwezi Juni 2017, Halmashauri ilitangaza nafasi za vyombo hivyo kwa ajili ya kuvihuisha kwani vyombo hivyo huishwa kila baada ya miaka mitatu kisheria.
Akiwahutubia wajumbe hao Mwenyekiti wa Halmashauri aliwasisitiza wajumbe hao waoneshe kuelewa na kuwa tayari kushiriki katika maendeleo ya sekta ya afya katika Halmashauri yetu kwani wapo kisheria.
Mh. Kibiki alisema kuwa mwaka 1994 Wizara ya Afya ilitengeneza utaratibu wa mabadiliko katika sekta ya afya. Mkakati mkuu katika mabadiliko haya ni kurejesha madaraka ya uendeshaji huduma katika Halmashauri na katika ngazi ya chini kabisa ya jamii kwa kuanzisha Bodi za Huduma za afya na Kamati za Usimamizi za vituo vya huduma za afya ambazo zitafanya kazi chini ya Halmashauri za serikali za mitaa.
Bodi ya afya inawajibika kwa Halmashauri na ina kazi zifuatazo:
i. Kujadili na kurekebisha mipango ya Afya na bajeti na kuiwasilisha kwa Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa;
ii. Kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji kutoka kwa Timu za Uendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri;
iii. Kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na kukusanya rasilimali za kutosha kuendesha huduma za Afya za Halmashauri;
iv. Kushirikiana na Kamati za Afya za Vituo, washirika wengine kwa nia ya kuinua kiwango cha Afya na utoaji wa huduma;
v. Kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya Afya katika eneo la mamlaka husika.
vi. Kuisaidia Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri katika kusimamia rasilimali za Afya
vii. Kuimarisha miundombinu endelevu na mfumo wa mawasiliano na usambazaji.
viii. Kuhakikisha kunakuwepo wafanyakazi kulingana na ikama ya Halmashauri.
Kamati ya Usimamizi ya Hospitali itatekeleza majukumu kama hayo kwa ngazi ya Hospitali.
A: Wajumbe wa bodi ya afya
1. Wilson Abong’o – Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
2. Hilda Njidile - Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
3. Ulumbi Kitundu - Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
4. Monica Mollel - Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
5. John Kitale - Mwakilishi kutoka Taasisi/Asasi za Kijamii (NGOs na FBOs)
6. Julieth Fransis - Mwakilishi kutoka watoa huduma za afya binafsi.
7. Jane Wado - Mwakilishi kutoka Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Mkoa
Wajumbe wengine wanne wataingia kwa nyadhifa zao .
8. Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii
9. Mganga Mkuu wa Halmashauri
10. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji wa Babati
11. Afisa Mipango wa Halmashauri
B: Wajumbe wa kamati ya Usimamizi wa Hospitali
1. Latifa Ally Juma – Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
2. Emmanuel Mathew - Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
3. Toto Mohamed - Mwakilishi kutoka ngazi ya jamii
4. Emmanuel Dohho - Mwakilishi kutoka kamati za vituo vya afya
5. Alhaji Ramadhani - Mwakilishi kutoka kamati za zahanati za serikali
6. John Mumbray - Mwakilishi kutoka Taasisi/Asasi za Kijamii (NGOs na FBOs)
7. Michal Nkya - Mwakilishi kutoka watoa huduma za afya binafsi.
8. Edastella Ndowo - Mwakilishi toka Halmashauri aliyeteuliwa na Mkurugenzi
Wajumbe wengine watatu wataingia kwa nyadhifa zao
9. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mji
10. Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Mji
11. Mwakilishi toka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mji (CHMT)
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati