Baraza la Madiwani lililokuwa lililokutana leo limeghairishwa hadi siku ya Alhamis tarehe 16/11/2017 kutokana na hoja iliyotolewa na Mh.Manfred Diwani wa Mutuka.
Wakichangia hoja hiyo madiwani hao walikubaliana na hoja ya kughairishwa kwa Baraza ili kuwapa Madiwani muda wa kupitia mapendekezo ya sheria hizo kwa ajili ya manufaa ya wana Babati.
Baada ya Mjadala wa kina wajumbe nane kati ya tisa waliohudhuria walikubaliana na hoja ya kughairisha kikao hicho na Mjumbe mmoja alikataa.
Akighairisha Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Kibiki M. Kibiki aliwataka wajumbe wawe wamoja katika mambo yanayohusu maendeleo ya Halmashauri yao na kuwasisitiza kwenda kuzisoma kwa umakini ili wakikutana wazipitishe ili zipate kutumika katika Mji wa Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati