Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati anawataarifu waombaji kazi kwa nafasi ya Makatibu Mahsusi Daraja la III na Madereva Daraja II kuwa usaili umepangwa kufanyika
siku ya Jumanne tarehe 28/06/2022 Saa 2:00 Asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Babati.
Wasailiwa wote wanatakiwa kuja na vyeti halisi (Original) vifuatavyo:-
A: MAKATIBU MUHSUSI DARAJA LA III
1. Cheti cha kuzaliwa.
2. Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI).
3. Kitambulisho cha NIDA.
4. Cheti cha Uhazili chenye ufaulu wa mtihani wa hatua ya tatu.
5. Cheti cha Kompyuta katika program za Windows,Microsoft Office,Internet, E-mail na Publisher
B:MADEREVA DARAJA II
1. Cheti cha kuzaliwa.
2. Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI)
3.Kitambulisho cha NIDA.
4. Leseni ya udereva ya Daraja E au C1 ya mwaka mmoja (1).
5. Cheti cha mafunzo ya Msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course).
6. Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II waje nacho.
Pamoja na tangazo hili orodha ya waombaji wenye sifa kwa ajili ya kuhudhuria katika usaili imeambatishwa.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati