Na Nyeneu, P. R - Mjini Babati
Mradi wa BOOST ni mradi wa kuimarisha na kuboresha elimu ya awali na msingi hapa nchini ambao una thamani ya Tsh Trilioni 1.15. Mradi huu unatekelezwa nchini kwa muda miaka 5 hivyo kukamilika mwaka 2025/2026 na umelenga kunufaisha Halmashauri zote 184 nchini hususani katika kuboresha miundombinu ya elimu kwa Madarasa ya awali na Msingi.
Tarehe 27 Aprili, 2023 Halmashauri ya Mji wa Babati imepokea fedha za Mradi huu wa BOOST jumla ya Shilingi 661,500,000 kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa, Matundu ya vyoo katika shule za msingi za Hangoni, Komoto, Kwaang’w na Kiongozi na ujenzi wa shule mpya ya Mfano ya mkondo mmoja katika shule ya msingi Sinai.
Katika fedha hizo, Shule ya Msingi Hangoni imepokea fedha jumla ya shilingi 69,100,000 kwaajili ya Ujenzi wa vyumba 02 vya madarasa ya mfano ya Elimu ya Awali, matundu 06 ya vyoo (yakiwemo 02 ya wanafunzi wenye mahitaji maalum). Shule za Msingi za Komoto, Kwaang’w na Kiongozi zimepokea jumla ya shilingi 81,300,000 kwa kila shule kwaajili ya ujenzi wa madarasa 3 na matundu 3 ya vyoo.
Vilevile Shule ya Msingi Sinai imepokea fedha shilingi 348,500,000 kwaajili ya ujenzi wa shule ya Mfano ya Mkondo mmoja ambapo utahusisha vyumba vya madarasa 02 vya mfano vya Elimu ya Awali vyenye matundu 06 ya vyoo vya Elimu ya Awali (matundu 2 kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na matundu 4 kwaajili ya wanafunzi wasio na mahitaji maalumu), vyumba 07 vya madarasa, matundu 10 ya vyoo (02 walimu na 08 wanafunzi), jengo la utawala, na kichomea taka kwa Shule ya Msingi.
Aidha, mradi huu ni wa Lipa kwa Matokeo (P for R), hivyo, inaelekezwa kukamilisha kwa wakati na kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa ili Serikali iendelee kupata fedha za ujenzi kupitia Mradi wa BOOST.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati