Afisa Mwandikishaji Jimbo la Babati Mjini Bi.Edna Moshi amefungua rasmi mafunzo kwa waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi katika Shule ya Sekondari Babati Day Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura litaanza tarehe 04/09/2024 – 10/09/2024 katika Vituo takribani 64 vilivyopo ndani ya Kata 8.
Mafunzo hayo yameudhuriwa na Bi.Mariam Kiravu Afisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Msimamizi wa Mkoa wa Manyara,Wataalam wa TEHAMA kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Aro Jimbo na Aro Kata,Mwenyekiti wa Mafunzo,Wakufunzi wa Mafunzo ,Maafisa Uchaguzi na Maafisa Ugavi.
Bi.Edna Moshi amesema kuwa takribani Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa vifaa vya Bayomertiki 158 wamepatiwa mafunzo ambayo yanalengwa kuwajengea umahiri zaidi na ndio wahusika wa uandikishaji wa wapiga kura vituoni.Na amewasisitiza kuvitunza vifaa ambavyo watakabidhiwa wakati wa zoezi hilo na kufanya kazi kwa umakini vituoni.
Vilivile amesema kuwa katika uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhuiswa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura lakini mawakala au Viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kituoni.
Aidha ameongeza kuwa Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa Uboreshaji wa Daftari kwa Asasi za kirai 157 na asasi 33 za kirai kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo.
Sambamba na hilo Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi wasaidizi wameapa mbele ya Afisa mwandikishaji Jimbo la Babati kuwa watafanya kazi kwa umakini,watakuwa watii na weledi wakati wote katika zoezi hilo la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati