• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumisha
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

TASAF yazindua mfumo mpya wa malipo kwa Walengwa

Imechapishwa: December 18th, 2020

Na Nyeneu, P. R - Mjini Babati

“TASAF ipo katika mchakato wa kubadili njia ya malipo kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini ili kuhawilisha ruzuku kwa njia ya kielektroniki na kuondokana na njia ya kulipa taslimu.” Alisema Bw. Edmund Mwalongo (Mwezeshaji kutoka TASAF Makao makuu) kwenye mafunzo ya kuwawezesha wawezeshaji ngazi ya Halmashauri yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati. Mafunzo haya yanayofanyika nchi nzima yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wawezeshaji kuwaandikisha walengwa wote katika njia ya malipo kwa mtandao yaani e-Payment ambapo walengwa wanatakiwa kuwa na akaunti za simu au benki.

Mpango huu umetekelezwa kwa majaribio katika maeneo ya mamlaka ya utekelezaji 19 Tanzania Bara na Visiwani ambazo ni asilimia 10 ya mamlaka zote 181 zilizopo. Mamlaka hizo ni Bahi, Kisarawe, Mkuranga, Unguja, Kilwa, Siha, Bagamoyo, Mpanda Mji, Arusha Mjini, Kigoma Manispaa, Songea Manispaa, Muheza, Temeke, Kinondoni, Ilala, Ubungo, Kigamboni, Chalinze na Urambo. Majaribio haya yalianza mwezi Mei/Juni 2017.

Jumla ya walengwa kabla ya uhakiki katika mamlaka hizo walikuwa 101, 568, baada ya uhakiki idadi ya walengwa katika PAA hizo ni 73,911. Ili kuweza kufanikisha zoezi hili la uandikishaji wa Wakilishi, ni lazima mlengwa awe amekizi vigezo vifuatavyo:-

1. Awe mwakilishi wa kaya na sio mkuu wa kaya

2. Awe na akaunti iliyosajiliwa katika huduma ya benki au huduma za kifedha za simu

3. Jina lililosajiliwa katika mpango lifanane na jina lililosajiliwa kwenye akaunti ya simu au benki

4. Ajaze na kusaini fomu ya maombi (concent form) ya kujiunga kupokea malipo kwa njia ya mtandao

5. Akaunti ithibitishwe uhai wake na jina lililosajiliwa katika huduma ya benki au huduma za kifedha za simu.

Aidha, Katika kipindi hiki  uhamasishaji na kuwawezesha  wawakilishi wa kaya ambao hawana akaunti kufungua akaunti  mpya za benki au akaunti za simu ambazo zitawawezesha kupokea fedha  kwa kipindi cha malipo ya  Nov/December umefanyika na unaendelea kufanyika awamu kwa awamu. Takwimu  hizo zitakusanywa na zitahakikiwa ili ziweze kutumika kwa  malipo yajayo yaani yatakayofanyika kwa kipindi cha November/December. Muwezesha aliendelea kusisitiza kuwa utaratibu wa malipo ya kielektroniki uelezwe bayana kwa wawakilishi  wa kaya zote na kujaza fomu ya kujiandikisha(consent form). Hata hivyo, kwa kujaza na kusaini fomu ya uthibitisho wa malipo ya kielektroniki au fomu ya malipo ya kielektroniki, wawakilishi wa kaya watakuwa wamethibitisha na kutoa idhini  ya kulipwa kupitia simu au benki akaunti. Pia watakuwa wamewaruhusu TASAF kuwasiliana na benki au watoa huduma ili kuwaomba  uthibitisho wa taarifa za akaunti zao walizotoa, kwani yote haya yanafanyika kwaajili ya kuimarisha utoaji huduma kwa walengwa.

Pamoja na hayo, utambuzi wa walengwa kwa njia ya vidole (Proper identification/authentication) ni moja ya hitaji muhimu la kufanikisha malipo kwa njia ya OTC(Over The Counter) na ili malipo kwa njia ya OTC yaweze kufanikiwa ni lazma kila mlengwa awe na number ya NIDA yaani amejisajili NIDA. Pia, ili kufanikisha hili, TASAF imekuwa ikishirikiana na NIDA kuhakikisha walengwa wote wanaandikishwa na kupewa number za utambulisho NIN (National Identification Number) hivyo kuwalazimu walengwa wote ambao hawajawasilisha/hawajajiandikisha wanatakiwa kufanya hivyo na NIN zote kwa utaratibu mzuri zitachukuliwa na kuingizwa kwenye mfumo wa e-Payment.

Bw. Malongo aliendelea kutoa mafunzo na kueleza malengo na faida ambazo mlengwa angepata katika malipo kwa njia ya mtandao, kama ifuatavyo;

  • Malipo kwa njia ya mtandao ni njia Salama kabisa katika fedha za mlengwa. Malipo kwa njia ya kielektroniki yataondoa athari zinazoweza kutokea wakati wa kusafirisha fedha taslimu kuelekea maeneo ya malipo

  • Huleta fursa zaidi ya kufanya maamuzi sahihi kabla ya kutumia. Malipo kwa njia ya e-Payment yataleta fursa kwa walengwa kifikiri na kufanya maamuzi sahihi katika matumizi ya huduma za kifedha ili kuboresha maisha yao mfano Kulipia Bima, Kuweka akiba na kulipia huduma mbalimbali.

  • Kupata pesa kwa wakati na popote alipo mlengwa bila kusubiri na kupanga foleni. Hii itawawezesha walengwa kupokea pesa moja kwa moja katika akaunti zao za simu au benki, mahali popote walipo bila kusubiri na kupanga foleni.


  • Kupata muda zaidi wa kufaya shughuli za maendeoleo

  • Pia kupunguza gharama za kusafirisha fedha kwa magari kuelekea maeneo ya malipo.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 BABATI MJI December 18, 2020
  • ORODHA YA WASIMAMIZI WA VITUO, WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO NA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA October 20, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • TANGAZO KWA WALE AMBAO HAWAJAENDELEZA MAENEO YA KUJENGA VIBANDA UWANJA WA KWARAA August 15, 2020
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Baraza la Mtihani (NECTA) latangaza matokeo - CSEE, FTNA, QT na SFNA

    January 15, 2021
  • TASAF yazindua mfumo mpya wa malipo kwa Walengwa

    December 18, 2020
  • Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi amshukuru Mhe. Rais Mbele ya Baraza la Madiwani Mjini Babati

    December 11, 2020
  • Karibuni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino - DC Twange

    November 28, 2020
  • Tazama zaidi

Video

MWENGE WA UHURU 2018 KARIBU BABATI MJI.
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati