Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe amefanya ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Mji na wilaya ya Babati kwa kuongea na watumishi na kutembea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kabla ya kutembelea miradi Katibu Mkuu aliongea na watumishi wote wa Halmashauri zote mbili siku ya Ijumaa tarehe 09/02/2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na kuwataka watumishi kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Pia aliwasisitiza Maafisa Utumishi katika Halmashuri wawatendee haki watumishi kwa kuwapa stahili zao ikiwa ni pamoja na ruhusa za kwenda kusoma, uhamisho n.k
Katika mkutano huo na watumishi Katibu Mkuu aliwahakikishia watumishi wote wenye madai yao kulipwa na serikali baada ya madai hayo kuhakikiwa.
Siku ya pili ya ziara ya Katibu Mkuu alitembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuona hatua zilizofikiwa kukamilisha miradi. Katika miradi hiyo alizitaka Halmashauri kuanzisha shule za Sayansi kwa kidato cha Tano na cha Sita na TAMISEMI ipo tayari kuwaunga mkono,Madarasa yajengwe njia za kupita kupita walemavu na aliwataka wafadhili wanaojenga shule wafuate ramani iliyowekwa ili madarasa yote yawe na muonekano unaofanana.
Katika mradi wa Barabara za lami Mhandisi Iyombe aliipongeza Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kujenga Barabara nzuri za kisasa na zenye viwango lakini aliwashauri ujenzi huo uambatane na uwekaji wa taa za Barabarani ili nyakati za usiku kuepusha ajali za barabarani na uhalifu wa aina mbalimbali nyakati za usiku.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati